1 Chronicles 24

Migawanyo Ya Makuhani

1 aHii ndiyo migawanyo ya wana wa Aroni:

Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
2 bNadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao, nao hawakuwa na wana; kwa hiyo ndugu zao Eleazari na Ithamari wakahudumu kama makuhani. 3 cAkisaidiwa na Sadoki mwana wa Eleazari na Ahimeleki mwana wa Ithamari, Daudi aliwapanga wazao wa Aroni katika migawanyo kufuatana na wajibu wa huduma zao. 4Idadi kubwa ya viongozi walipatikana miongoni mwa wazao wa Eleazari, kuliko miongoni mwa wazao wa Ithamari, nao waligawanywa kwa uwiano: Viongozi kumi na sita kutoka jamaa ya wazao wa Eleazari na viongozi wanane kutoka jamaa ya wazao wa Ithamari. 5 dWaliwagawanya bila upendeleo kwa kupiga kura, kwa kuwa kulikuwa na maafisa wa mahali patakatifu na maafisa wa Mungu miongoni mwa wazao wale wa Eleazari na wale wa Ithamari.

6 eMwandishi Shemaya mwana wa Nethaneli, Mlawi, aliorodhesha majina yao mbele ya Mfalme Daudi na maafisa: Kuhani Sadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa jamaa za makuhani na za Walawi: jamaa moja ikitoka upande wa Eleazari na nyingine upande wa Ithamari.

7 fKura ya kwanza ilimwangukia Yehoyaribu,
ya pili Yedaya,
8 gya tatu Harimu,
ya nne Seorimu,
9ya tano Malkiya,
ya sita Miyamini,
10 hya saba Hakosi,
ya nane Abiya,
11ya tisa Yeshua,
ya kumi Shekania,
12ya kumi na moja Eliashibu,
ya kumi na mbili Yakimu,
13ya kumi na tatu Hupa,
ya kumi na nne Yeshebeabu,
14 iya kumi na tano Bilga,
ya kumi na sita Imeri,
15 jya kumi na saba Heziri,
ya kumi na nane Hapisesi,
16ya kumi na tisa Pethahia,
ya ishirini Yehezkeli,
17ya ishirini na moja Yakini,
ya ishirini na mbili Gamuli,
18ya ishirini na tatu Delaya,
ya ishirini na nne Maazia.

19 kHuu ulikuwa ndio utaratibu wao uliokubalika wa kuhudumu walipoingia katika Hekalu la Bwana kulingana na masharti waliyoelekezwa na Aroni baba yao, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyokuwa amemwamuru.

Walawi Waliobaki

20 lKuhusu wazao wa Lawi waliobaki:

Kutoka kwa wana wa Amramu: alikuwa Shubaeli;
kutoka kwa wana wa Shubaeli: alikuwa Yedeya.
21Kwa wa Rehabia, kutoka kwa wanawe:
Ishia alikuwa wa kwanza.
22Kutoka kwa Waishari: alikuwa Shelomithi,
kutoka kwa wana wa Shelomithi: alikuwa Yahathi.
23 mWana wa Hebroni: Yeria alikuwa mkuu, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
24Mwana wa Uzieli: alikuwa Mika;
kutoka kwa wana wa Mika: alikuwa Shamiri.
25 nNdugu yake Mika: alikuwa Ishia;
na kutoka kwa wana wa Ishia: alikuwa Zekaria.
26 oWana wa Merari: walikuwa Mahli na Mushi.
Mwana wa Yaazia: alikuwa Beno.
27Wana wa Merari:
kutoka kwa Yaazia: ni Beno, Shohamu, Zakuri na Ibri.
28 pKutoka kwa Mahli: alikuwa Eleazari, ambaye hakuwa na wana.
29Kutoka kwa Kishi: mwana wa Kishi:
alikuwa Yerameeli.
30 qNao wana wa Mushi: walikuwa Mahli, Ederi na Yeremothi.

Hawa walikuwa Walawi kulingana na jamaa zao.
31Pia walipiga kura kama vile ndugu zao wazao wa Aroni walivyofanya, mbele ya Mfalme Daudi, Sadoki, Ahimeleki na mbele ya viongozi wa jamaa ya makuhani na ya Walawi. Jamaa za ndugu wakubwa zilitendewa sawasawa na zile za ndugu wadogo.

Copyright information for SwhNEN